Naibu
Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),
Joseph Kakunda imesema kuwa zipo idara nyingi ambazo zinaweza kuwasaidia
vijana kujikwamua ili kuendeleza biashara kama kujiunga katika idara ya
vijana kwenye Halmashauri.
Kauli
hiyo imetolewa na Kakunda jana, Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge
wa Viti Maalum (CCM)Zainab Katimba, aliyehoji “Kwa kuwa jitihada za
kutoa mitaji kwa vijana na wanawake inabidi ziende sambamba na
kuwajengea uwezo wa kuanzisha na kuendeleza biashara, Je serikali ina
mkakati gani wa kuwatumia hawa maafisa Biashara katika kuwajengea uwezo
vijana wanaokuwa katika vikundi ambao wananufaika na asilimia 10
inayotengwa kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri?
“Nataka
nikuhakikishie kwamba vijana katika nchi hii wana idara nyingi sana za
kuweza kuwasaidia mawazo ya kujikwamua kutoka pale walipo kutoka kwenda
mbele, kuna idara ya vijana katika Halmashauri kuna idara katika
maendeleo ya jamii, kuna idara ya mipango sasa Maafisa Biashara
tunawaongezea sehemu nyingine,” alisema Kakunda.
“Kwahiyo
mimi napenda nitumie nafasi hii kuwaomba vijana wa nchi hii kutumia
fursa ambazo zipo katika Halmashauri wamekuwa hawazitumii ipasavyo,
ukienda katika Halmashauri unaona maombi ya vijana yako asilimia 10 ya
maombi yote yaliyowasilishwa naomba tujitahidi sisi Wabunge kuwaelimisha
kuwaomba vijana wajitokeze katika vikundi na watumie fursa zilizopo
kwaajili ya kujiendeleza na serikali tuko macho kuhakikisha jambo hilo
linatekelezwa vizuri.”
Mpekuzi.
Comments