Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wananchi hasa wanaume kupima Virusi vya
Ukimwi na wale wenye maambukizi waanze dawa mapema.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo jana Juni 27 wakati wa uzinduzin wa vituo 51
vinavyojitegemea vya kupima hali ya hewa, Wilayani Bahi, Dodoma.
“Ugonjwa
wa Ukimwi ni hatari na hatari zaidi ni pale wananchi tunapotembea
tukiwa hatujiju kama tuna VVU ama hatuna, kwa hiyo mipango ya Serikali
ni kila mmoja bora ajijue afya yake kwa kwenda kupima,”alisema.
Pia
amewataka viongozi mbalimbali watakapoandaa mikutano yenye zaidi ya
watu mia moja kuweka vibanda kwa ajili ya kupima kwani huduma huyo haina
gharama.
“Nahamasisha
wote kuanzia watumishi na wananchi wote kupima afya zao, tunataka
ifikapo mwaka 2020 asilimia 90 ya wananchi wawe wanazijua afya zao hasa
wanaume,”alisema na kuongeza:
“Na
kwa wale wataokutwa na maambukizi waanze kutumia dawa na uzuri sasa
hivi hizi dawa zinaanza kutumiwa mara tu baada ya kugundulika
umeathirika.”
Majaliwa
ameiagiza Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Wizara ya Uchukuzi na
Mawasiliano kutenga fedha kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa mradi
wa vituo vya hali ya hewa ili wananchi wapate taarifa za hali ya hewa
katika maeneo mbalimbali nchini.
Pia
amewaagiza wataalamu wa sekta mbalimbali kutumia taarifa za hali ya
hewa katika kazi zao ikiwemo kutoa taarifa mbalimbali kwa wakulima na
kushauri maeneo gani wanaweza kufanya kilimo.
Mpekuzi.
Comments