Makamu Mwenyekiti wa chama cha ADA TADEA, Juma Ali Khatib, alisema Dk. Shein ametekeleza matakwa ya kikatiba kwa kuwashirikisha viongozi wa vyama vya siasa katika uteuzi wa tume hiyo na kwamba wameridhishwa nayo.
Alisema chama chake hakina shaka na Mwenyekiti mpya wa ZEC Jaji Mkuu Mstaafu, Hamid Hamid Mahmoud kwani mbali ya uzoefu wake lakini ni mtu mwenye kutenda haki.
Alisema anaamini uzoefu alionao Mwenyekiti huyo kama atautumia, hakuna shaka nchi itakuwa kwenye amani baada ya kumalizika chaguzi.
Makamu huyo alisema chama chake, hakina wasi wasi na uongozi na tume mpya, licha ya kuwa hakuna mpizani kutoka ndani ya chama chao, lakini walioteuliwa kuunda tume hiyo wataweza kuwawakilisha vizuri.
Zanzibarleo.
Comments