Mwenyekiti
Mwenza wa Ukawa, James Mbatia, amesema endapo serikali haitatoa fedha
za mauzo ya korosho, Umoja huo wa Katiba ya Wananchi utakwenda
mahakamani kudai haki hiyo.
Mbatia
alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Viwanja
vya Bunge jijini Dodoma jana akiwa na wabunge wa vyama vinavyounda
Ukawa.
Umoja huo unaundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.
Mbatia
ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), alisema watazitumia siku
mbili zilizobaki za Bunge la Bajeti kudai bungeni malipo hayo ya korosho
na endapo serikali haitatoa fedha hizo, watalazimika kuisaka haki hiyo
nje ya Bunge kwa kufunga kesi mahakamani.
"Korosho
ambayo ilikuwa inatuingizia fedha za kigeni ni wazi sasa uchumi wa
taifa letu utazidi kudidimia na ukididimia wote tunaumia," Mbatia
alisema na kuongeza:
"Sasa
tutaendelea kupinga bungeni wakati wa mjadala wa 'Finance Bill'
(Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2018), hiyo sheria inayotaka
kupokonya haki za wakulima, ikishindikana tutaidai haki hii mahakamani."
Mbatia
alisema serikali inapaswa kuwa makini kwa kuwa taifa linapokuwa
limepasuka na watu wake kuwa na hofu, haliwezi kuwa na maendeleo.
"Jambo
hili la korosho ni kubwa na tusipolisimamia vizuri hatutafika pazuri.
Kwenye Finance Bill, serikali ihakikishe wakulima hawa wa korosho
wanapata haki zao za msingi," alisema Mbatia huku akieleza kuwa wanaunga
mkono hoja ya Mbunge wa Kilwa Kusini, Seleman Bungara 'Bwege' (CUF)
kuitisha maandamano kudai fedha hizo.
Naye
Mbunge wa Malindi, Ally Saleh (CUF), alisema kitendo cha serikali
kutotoa fedha hizo za wakulima ni kuvunja sheria na wawekezaji wataogopa
kuja nchini.
“Serikali
inapothubutu kuondosha fedha za wakulima ambazo zipo kisheria,
tunapeleka ujumbe mbovu kwa wawekezaji. Sasa hivi tunataka kujenga
viwanda na kukaribisha wawekezaji, ina maana kwamba hatuheshimu sheria,
hivyo wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza," alisemana kuongeza:
“Serikali
inashindwa kuwekeza kwenye zao ambalo ni 'the best' (bora zaidi) katika
nchi kwa sasa na inasema inashawishi watu waje wawekeze viwanda vya
kubangua. Je, utamleta nani aje awekeze ikiwa serikali haiaminiki?
Nadhani serikali inapaswa kuwa makini sana katika hili."
Naye
Mbunge wa Mchinga, Hamidu Bobali (CUF), alisema hakubaliani na maelezo
yaliyowasilishwa bungeni Jumatatu na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk.
Adelardus Kilangi, kuwa serikali haitolipa fedha hizo kwa sababu za
kisheria na kwamba wanayo nakala ya hukumu ya mahakama inayoonyesha
serikali ilishindwa katika kesi dhidi ya Bodi ya Korosho na kutakiwa
kulipa fedha hizo.
Katika
maelezo yake bungeni, Dk. Kilangi alisema fedha hizo ni za umma na
kwamba Bodi ya Korosho inakusanya kwa niaba ya serikali na kupanga
matumizi.
“Msimamo
huo umetokana na uamuzi wa kesi zilizofunguliwa kwenye Mahakama Kuu na
Mahakama ya Rufaa na haujawahi kupingwa," alisema na kuongeza kuwa:
“Serikali
haiwezi kulipa fedha kwenye mfuko ambao haujaanzishwa kwenye sheria
ambayo haijatungwa na Bunge. Endapo serikali ikifanya kinyume cha hapo,
itakuwa imevunja sheria."
Mpekuzi.
Comments