
Hayo yanakuja kufuatia tangaazo la hivi karibuni la TCRA, la kuwataka wamiliki wa mitandao hayo kuisajili haraka vyenginevyo hawataruhusiwa kutoa huduma.
Baadhi ya mitandano, ukiwemo mtandao maarufu wa Jamii Forum, umesitisha kutoa huduma kutokana na tangazo hilo la TCRA.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Meneja wa TCRA kanda ya Zazibar, Esuvatie Aisa Masinga, alisema wamiliki wa mitandao hiyo waliopo Zanzibar, wasiwe na wasiwasi kwamba watawajibika kwa TCRA kama wengine wanavyofikiria.
Alisema waendelee kufanya kazi zao kwa ufanisi na wala wasiwe na wasi wasi kwamba TCRA itaingilia kati.
Zanzibar24.
Comments