RC Ayoub afanya uteuzi wa masheha Mjini Magharibi Unguja.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh Ayoub Mohamed Mahamoud ametengua uteuzi wa sheha wa shehia ya Kiembesamaki Bw. Maulid Ali Maulid na badala yake kumteua Bw. Shaka Khatibu Juma kuwa sheha wa shehia hiyo  kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu namba 9 cha sheria ya Tawala za Mikoa namba 8  ya mwaka 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo katibu Tawala Mkoa wa Mjini Magharibi Bi Hamida Mussa Khamis hapo ofisini kwake Vuga amesema hatua hiyo imefanyika kutokana na sababu ya sheria hiyo na miongozo ya kiutendaji ya imeelekeza sifa za masheha na uwezo wa mammlaka za uteuzi huo.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameteuwa Bi Asha Ali Ali kuwa sheha wa shehia ya Kikwajuni juu  ,Bwana Gharibub Ali Kombo kuwa Sheha wa shehia mpya ya Mwembe Madema na Nd Soud Rajab Soud kuwa Sheha wa Shehia ya Matarumbeta ambayo ilikuwa wazi kufutia kufariki kwa sheha wa shehia hiyo.

Pia Mkuu wa Mkoa amemteuwa Bw Hassan Masoud Ali kuwa Sheha wa Shehia Malindi kushika nafasi ya Nd Ramadhani Haji Mussa ambae ameomba kutenguliwa uteuzi wake kutokana na afya yake kutokua nzuri kulingana na majukumu ya kazi hiyo nakuomba uongonzi wa mkoa nafsi hiyo kumpatia wananchi mwengine ambapo aliteuliwa tarehe 29/03/2018.

Kazi ya Uteuzi wa masheha hao imefanyika kutokana na sababu mbali mbali zikiwemo nafasi tupu shehia kutokuwa na sheha maradhi,kifo na sababu nyengine za uwajibikaji ambapo uteuzi huo umeanza  tarehe 27 juni 2018.

Mzee  George.
kutoka ofsi ya mkuu wa mkoa mjini magharib
Zanzibar24.

Comments