RC Ayoub aahidi kuiunga mkono Serikali kwa hili.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud amesema serikali ya mkoa wa mjini itaendelea kushirikiana na serikali kuu ya mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya ambapo takwimu zinasema vijana takribani elfu 10 kwa Zanzibar  wameingia katika janga hili la matumizi ya dawa za kulevya.
Mhe. Ayoub ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku  ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani ambapo kwa Zanzibar yalifanyika katika viwanja vya Mapinduzi square.
Amesema “ tangu tuanze mapambano hayo kama serikali ya mkoa wa mjini magharibi  tumefanikiwa kukamata na kubaini jumla ya kesi 426 ambapo kesi 157 zilipelekwa katika vyombo husika vya sheria kwa ajili ya maamuzi zaidi”.
Hata hivyo alisema changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili na kupelekea kukwama kwa kesi ni uelewa mdogo kwa baadhi ya watumishi kama vile Jeshi la Polisi na hata wafanyakazi wa tume inayoshughulikia udhibiti wa dawa za kulevya nchini.
Maadhimisho hayo ya kupiga vita matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya duniani huadhimishwa kila ifikapo juni 26 ya kila mwaka ambapo kaulimbiu ya mwaka huu “TUENDELEZE MAISHA YETU, JAMII YETU NA UTAMBULISHO WETU, BILA DAWA ZA KULEVYA”.
Zanzibar24.

Comments