
Katika taarifa iliyotolewa leo Juni 20, 2018 na Ofisi ya Katibu wa
Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee,
imesema Rais Dkt. Shein, amefanya uteuzi huo chini ya kifungu 119 cha
katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984.
Pamoja na hayo Rais Dkt. Shein amefanya uteuzi wa wajumbe wengine
sita wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ambao ni Mabruki Jabu Makame,
Feteh Saad Mgeni na Makame Juma Pandu, wengine ni Dkt. Kombo Khamis
Hassan, Jaji Khamis Ramadhani Abdula na Bi Jokha Khamis Makame.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa wajumbe wote walioteuliwa wanatakiwa
kufika Ikulu ya Zanzibar, Ijumaa Juni 22, 2018 saa 4:00 asubuhi kwaajili
ya kuapishwa.
April 18, 2018 aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar,
Jecha Salim Jecha alitangaza kustaafu baada ya kumaliza muda wake kama
mwenyekiti wa tume hiyo baada ya kuhudumu kwa kipindi cha miaka mitano
tangu April 30, 2013.
Zanzibar24.
Comments