Rais
mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa amesema uzalishaji wa umeme
jua hapa nchini utachangia kuepukana na changamoto ya uharibifu wa
Mazingira.
Kauli
hiyo ameitoa jana Juni 19, 2018 jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi
wa Kitabu cha Mafunzo ya Umeme wa Jua uliofanyika Tume ya Sayansi na
Teknolojia (Costech).
"Kinachohitajika
kwa sasa ni kuweka mipango madhubuti na kuitekeleza, lakini ili
kufanikisha hilo, tunahitaji taasisi muhimu za Serikali kama Costech
kusimamia mipango hiyo kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo na
wataalamu mbalimbali kutoka serikalini na sekta binafsi,"alisema Mkapa.
Mkapa
alisema Sera ya Taifa ya Nishati ya Mwaka 2015, inaeleza wazi umuhimu
wa nishati ili kufikia uchumi endelevu na usioharibu mazingira.
Mpekuzi.
Comments