Polisi Mkoa wa Kusini Unguja La Toa Wito Kwa Madereva.

Madereva wametakiwa kutoendesha vyombo vyao ili kuepusha ajali kwa abiria wao pamoja na wanaokwenda kwa miguu barabarani.
Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Suleiman Hassan Suleiman wakati akizungumza  huko Ofisini kwake  Tunguu.

Amesema kuwa ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa kwa mwendo kasi wa magari hivyo ni vyema basi  madereva kuwajali abiria wao pamoja na wanaokwenda kwa miguu ili kuepushia athari zisizokua za lazima.

Kamanda suleiman amewasisitiza madereva kwenye mwezi huu mtukufu wa ramadhan na kuelekea sikukuu wawe na utaratibu au tabia ya kuendesha vyombo vyao kwa mwendo ambao hatouweza kumletea madhara na wala kumuathiri binaadamu na kuwataka kuheshimu sheria za barabarani.

Zanzibar24 

Comments