Serikali inakusudia kuifanyia marekebisho Sheria ya Sekta ya Korosho namba 203.
Kwa
mujibu wa muswada wa sheria ya fedha ya mwaka 2018, inapendekezwa
kufutwa mgawo wa fedha zinazotokana na ushuru wa kusafirisha korosho nje
zilizokuwa zikitolewa kwa wakulima ili kuboresha zao hilo.
Badala yake, muswada unapendekeza fedha hizo kupelekwa mfuko mkuu wa Hazina kama fedha nyingine za Serikali.
Sheria
ya sasa inataka asilimia 65 ya fedha zinazotokana na ushuru wa
kusafirisha korosho nje kupelekwa kwa wakulima kupitia Bodi ya Korosho
(CBT).
Fedha
hizo zilikuwa zikitumika kuendeleza kilimo cha korosho kama vile
kuendesha Chuo cha Utafiti Naliendele, kufanya utafiti wa mbegu bora na
kuzuia magonjwa ya mnyauko.
Muswada unapendekeza kifungu cha 17A kibadilishwe kwa kufuta kifungu kidogo cha (2) na kuingizwa kipengele kipya.
Kifungu
kipya kinachopendekezwa kinasomeka, “Mapato yote yatokanayo na ushuru
wa kusafirisha korosho yatahifadhiwa katika mfuko mkuu.”
Hivi
karibuni wabunge waliibana Serikali wakitaka kujua ziliko fedha
zinazotokana na mapato ya ushuru wa usafirishaji wa korosho nje.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Bajeti, Hawa Ghasia alitaka majibu ya Serikali, akisema
ripoti zinaonyesha fedha hizo zilizokusudiwa kuendeleza kilimo cha
korosho zimetumika katika matumizi mengine.
“Kukubali
mapendekezo haya ya mabadiliko ya sheria hii ni kuhujumu juhudi za
miaka mingi za kufufua zao la korosho, ni kuwatoa kafara wakulima wa
korosho nchini na kuhujumu mapato ya Serikali kwani korosho ndiyo zao
lililofanya vizuri msimu uliopita. Nitayapinga," amesema Nape katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.
Mpekuzi.
Comments