Muigizaji
wa Bongo movie maarufu kama Mwijaku amemmwagia povu zito msanii
mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake kusambaa siku ya jana.
Siku
ya jana Irene aliposti picha iliyozua utata Kwenye mitandao ya kijamii
na mara moja Mwijaku alimwandikia posti nzito ambayo alimsema sana kwa
vazi lile hasa kwa sababu ni mke wa mtu.
Lakini
Mwijaku hakuishia hapo kwani Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo
Tv, Mwijaku alionekana akiweka wazi Kuwa marafiki zake na a Uwoya
wanaomsapoti kwa picha zile ni wanafiki wakubwa kwani wanamshauri vibaya
wakijua wazi kabisa picha ile siyo nzuri:
"Irene
ni mtu mzima na mke wa mtu na hii ni ndoa yake ya pili kwa nini aposti
picha kama ile? Nikajiuliza Marehemu Ndikumana angekuwepo wakati amemuoa
angeweza kuposti kitu kama kile? Asingeweza kuposti Ndikumana alikuwa
mkali ila kwa sababu mume wake Dogo Janja ni mdogo basi anamuonea.
"Halafu
na marafiki wanaomzunguka Irene ni wanafiki siku akija kufa atakuwa
peke yake halafu na Shamsa Ford anaenda kumwambia hivyo hivyo umependeza
ishi utakavyo! Tuongee ukweli Shamsa Ford ni mnafki na anampoteza
mwenzake”.
Dogo
Janja ambaye ni mume wa Irene Uwoya aliweka wazi kuwa hakukerwa na
picha ile zaidi alimpa sapoti mke wake....Tazama Alichoandika
Comments