Mwanafunzi
wa darasa la tatu Shule ya Msingi Mlodaa, wilayani Chamwino, Asheri
Selemani (12), amefariki dunia baada ya kutahiriwa kienyeji.
Kwa
mujibu wa taarifa aliyoitoa kwa waandishi wa habari June 9 jijini
Dodoma, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, tukio hilo
limetokea katika kijiji cha Mlodaa kilichopo kata ya Mlowa barabarani.
Alifafanua kuwa mwanafunzi huyo alifariki dunia baada ya kuvuja damu nyingi kutokana na kutahiriwa kienyeji na ngariba.
Hata
hivyo, alisema baada ya tukio hilo ngariba huyo alitoroka na kutokomea
kusikojulikana na jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.
Katika
hatua nyingine, Jeshi la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu 35 kwa
tuhuma za kujihusisha na vitendo vya kihalifu katika maeneo mbalimbali
mkoani hapa.
Alifafanua
kuwa watu watatu wanashikiliwa kwa kuiba vifaa vya mafunzo ya Tehama
(tablet) 48 aina ya huawei na projekta moja zilizoibiwa katika Shule ya
Msingi St Gaspar ya Miyuji, jijini hapa.
Alitaja
thamani ya vifaa hivyo kuwa ni Sh. milioni 56 na vifaa hivyo ni vya
mradi maalumu wa mafunzo ya Tehama katika shule za msingi nchini na Mkoa
wa Dodoma mradi huo upo katika shule 10.
Alisema
vifaa hivyo vimekamatwa na jeshi hilo baada ya msako katika maeneo
mbalimbali mkoani hapa na vingine kukamatwa mikoa ya Dar es Salaam na
Arusha.
Aliwataja
watuhumiwa wanaoshikiliwa kwa kudaiwa kuhusika na tukio hilo kuwa ni
Nathanael Mkenda (25) mwanafunzi wa chuo cha madini,Timoth Mapunda (19)
fundi seremala na Benedict Mkinga (17) mwanfunzi kidato cha pili Shule
ya John Merlini.
Katika
tukio la pili, watuhumiwa wawili Peter Kihanda (28) mkazi wa Kahama
mkoani Shinyanga na Ramadhani Bakari Dereva wa lori namba T 105 CYL,
mali ya kampuni ya Simera Tansport Ltd., wanashikiliwa kwa kusafirisha
bangi vifurusi sita vyenye uzito wa kilo 162.
Hata
hivyo, Kamanda Muroto alisema katika tukio lingine walimkamata Manka
James, mkazi wa Isamilo mkoani Mwanza kwa kudaiwa kujihusisha na utapeli
wa kuwarubuni watu na kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu maeneo ya
benki.
Aidha,
alisema katika msako huo waliwakamata wahalifu wa kijihusisha na
ukabaji na uporaji nyakati za usiku katika maeneo mbalimbali ya jiji na
wengine wizi wa majumbani pamoja na pikipiki.
Muroto alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
Aliwashukuru
wananchi kwa kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na
kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao hivyo aliwaomba kuendelea kutoa
taarifa za wahalifu katika maeneo yao na jeshi hilo watazifanyia kazi.
“Jeshi
la Polisi tunafanya msako wa kuwatafuta wahalifu nyumba kwa nyumba hadi
sikukuu ya Idd itakapofika,tunataka wahalifu wakasherehekee sikukuu
hiyo wakiangalia kuta za magereza kwa sababu hawataki kuwa raia
wema”alisema Muroto.
Mpekuzi.
Comments