Mbunge
wa Ulyankulu (CCM), John Kadutu amesema ununuzi wa ndege za Bombardier
uliofanywa na Serikali hauna tija kwa wananchi wa jimbo lake iwapo
huduma za afya na barabara hazijaboreshwa.
Kadutu ametoa kauli hiyo jana Jumatano Juni 20, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19 bungeni mjini Dodoma.
Alisema
umebaki mwaka mmoja kabla ya nchi kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka
2020, hivyo ahadi zilizotolewa zinapaswa kutekelezwa.
“Serikali
imejenga reli, inanunua ndege hebu twendeni kwa wananchi, ujue ukienda
kule Ulyankulu ukauliza Bombardier hawakuelwi, barabara mbovu, afya
mbovu hawakuelewi,” alisema Kadutu.
“Pelekeni
fedha barabara ziboreshwe, Tarura (Wakala wa Barabara Mijini na
Vijijini) wapewe fedha. Bajeti iliyobaki ni moja ya kujadili kwa utulivu
kwani akili itakuwa majimboni tu, tusaidieni ili mwaka 2020 tupete,”
alisema.
Akigusia
ahadi za kampeni za uchaguzi, Kadutu alisema waliahidiwa jimbo la
Ulyankulu litakuwa wilaya lakini mpaka sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.
“Hamtaki
kutupa eneo lakini mnasema ahadi za Rais zitatekelezwa, sasa hii ni
ahadi ya Rais, alisema akiingia siku tatu tu tunapata wilaya,” alisema.
“Sasa
imebaki mwaka mmoja tu na nusu yako mengi, mmetuahidi lami tena
kilomita tatu tu lakini tunaona mambo ambayo hayako katika ilani
yanatekelezwa. Tukisema…,mimi watu wa Ulyankulu wamenituma.”
Mbunge
huyo amesema anashangazwa na mawaziri kutotembelea jimboni kwake huku
wakionekana kupishana katika majimbo mengine jambo linalokatisha tamaa
wananchi.
Mpekuzi.
Comments