Viongozi
9 wa CHADEMA, akiwemo Mwenyekiti wake Freeman Mbowe jana June 27, 2018
kupitia wakili wao wamewasilisha maombi chini ya hati ya dharura ya
kutaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu isitishe usikilizaji wa kesi yao
ya kufanya maandamano.
Maombi
hayo yanayotarajiwa kusikilizwa June 28, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbard Mashauri yamewasilishwa na wakili utetezi, Peter Kibatala.
Katika
maombi hayo namba 15/2018 upande wa utetezi umedai kuwa wanaomba
usikilizwaji wa kesi hiyo usitishwe hadi pale Mahakama Kuu
itakapoyapitia maamuzi yote yaliyotolewa na Mahakama ya Kisutu kuhusu
kesi hiyo.
Naye
Wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameiambia mahakama kuwa
wamepokea nakala ya maombi hayo, hivyo wanaomba kuwasilisha majibu yao
ya hati kinzani leo June 28, 2018.
Awali wakili Nchimbi alieeleza mahakama kuwa kesi hiyo imeitishwa ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali (Ph).
Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Mashauri ameiahirisha kesi ya msingi hadi July 2,2018.
Mbali
na Mbowe, washtakiwa wengine ni mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa,
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na
Mbunge wa kibamba John Mnyika.
Katibu
wa chama hicho Dk. Vicenti Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John
Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Tarime mjini Esther Matiko
na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.
Katika
kesi hiyo namba 112 ya mwaka 2018 Mbowe na wenzake hao wanaokabiliwa na
mashtaka 13 ikiwamo ya kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia,
kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi wa
uasi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai.
Makosa
hayo yanadaiwa kutendeka Februari 16,2018 katika maeneo ya viwanja vya
buibui, Mwananyamala na barabara ya Kawawa kinondoni mkwajuni.
Mpekuzi.
Comments