Alitoa ushauri huo hospitali kuu ya Mnazimmoja alipokuwa akiwakaribisha madakatari bingwa wa NEURO kutoka Marekani, Hispania na Abudhabi, ambao watakuwepo nchini kwa ajili ya kambi maalum ya matibabu ya maradhi hayo.
Alisema madaktari hao wanaotoka hospitali kubwa katika nchi zao ni wataalamu wazuri na iwapo wafanyakazi wa taasisi ya hospitali ya Mnazimmoja watakuwa wabunifu wanaweza kujifunza mambo mengi kutoka kwao.
Alisema kambi za mara kwa mara za matibabu ya madaktari bingwa kutoka mataifa mengine ni moja ya fursa kwa madaktari wa Zanzibar kujifunza na kuongeza utaalamu wao.
Aliahidi kuwa serikali itaendelea na juhudi za kuwasomesha madaktari wa taasisi NEURO nje ya nchi kila hali itakaporuhusu na kuiimarisha taasisi hiyo kwa lengo la kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje kwa ajili ya matibabu.
Zanzibarleo.
Comments