Istiqama Pemba yatoa msaada kwa wananchi.

Jumuiya ya kiislam Istiqama foundation iliyopo misufini Chake Chake  leo hii imefanikiwa kutoa misaada ya vipolo vya sabuni pamoja na vuiatu  kwa wananchi mbali mbali kisiwani Pemba.


Akizungumza na waumini wa kiislam kabla ya kuanza kwa harakati za kutoa misaada hiyo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Sheikh  Mohd Sleiman Taiwani amesema kuwa jumuiya imekuwa na utaratibu wa kutoa misaada kwa muda mrefu pale tu  Mwenyezi Mungu anapowajaalia kupata chochote kwao  hawana budi kuwafikiria wale wote ambao wanamazingira ya chini kwa mijini na vijijini.
Mwenye kiti wqa ISTIQAMA Pemba akikabidhi msaada.

Ameeleza kuwa kwa mika ya nyuma jumuiya hiyo ilikua ikifunga safari na kwenda kutoa misaada katika maeneo ya vijijini na kugundua kuwa kuna watu ambao wako ndani ya mji nao pia wanahitaji kupewa misaada.


Aidha Mwenyekiti huyo amesema ni vyema kwa wahisani kuangalia pia vijijini katika kutoa sadaka zao kwani  wako waumini wengi amabao wanahitaji kupewa misaada licha ya jumuiya hiyo kujitahidi katika suala hilo .


Amesema lengo la kutoa misaada hiyo nikutekeleza amri ya Mwenyezimungu kwa kuwafanyia ihsani kwa wale wasio jiweza.


Akizungumza kwa niamba ya Naibu Mufti Afisa Fatwa na Utafiti wa mambo ya kiislamu Pemba Sheikh Said Ahmed  Mohd amesema katika kutekeleza amri ya Mwenyezi mungu ni vyema kwa waumini kushindana katika mambo ya kheri ikiwemo kuwasaidi wale wasi jiweza hususan mayatima .


Kwa miaka kadhaa jumuiya ya kiislam ya Istiqama imekuwa ikishuhulika kutoa misaada mbali mbali kwa waumini katika kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hadi kufikia Skukuu ya Eid –l fitri.

Comments