Hamisa ambaye amewahi kuwa kwenye Mahusiano na Majizzo siku za nyuma na kuzaa naye mtoto mmoja ameweka wazi kuwa hivi sasa hana matatizo na Majizzo wala Lulu hivyo kwake ni Poa tu wakifunga ndoa.
Kwenye mahojiano na Risasi Jumamosi, Mobeto alisema kuwa hana kinyongo na Lulu kama ambavyo watu wanasema kwa kuwa mapenzi yake na Majizzo yalishakwisha siku nyingi.
"Mimi na huyo anayetaka kumuoa tulishamalizana, hivyo hakuna tena hata chembe ya mapenzi zaidi ya uhusiano wetu wa kulea mtoto.
"Kwa maana hiyo sina shida kusikia Lulu anaolewa na siku ya sherehe nikipewa kadi nitakwenda“.
Comments