Hamahama yaikumba Poland Kwa Kichapo Cha Bao 3-0 Dhidi Ya Colombia.

Poland imeyaaga mashindano ya Kombe la Dunia Urusi kwa kukubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Colombia.

Matokeo ya mchezo huo yamewekwa kimiani na Yerry Mina (40'), Radamel Falcao (70') na Juan Cuadrado dakika ya 75.

Poland inaondoka rasmi kwenye michuano kufuatia kupoteza mchezo wa pili mfululizo baada ya ule kwanza dhidi ya Senegal kuruhusu nyavu zao kufungwa mabao 2-1.

Msimamo wa kundi H unaonesha Colombia wapo nafasi ya tatu wakiwa na alama 3 huku Senegal wakishika nafasi ya pili, wakati Japan wakiwa wa kwanza.

Comments