Dkt. Shein azindua mfumo wa usajili mali na biashara kwa mtandao.

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar SMZ  itaendelea na jitahada mbali mbali za kuhakikisha wanakuza sekta ya habari na mawasiliano Tehama ili kuwanufaisha wazanzibar na watanzania kwa ujumla.
Hayo aliyabainisha katika hafla maalum ya uzinduzi wa mfumo wa usajili kwa kutumia mtandao kwa tasisi za biashara na amana kwa mali zinazohamashika  Dokta Shein amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuchukua hatua hizo ambazo   zitasaidia kuleta tija na kukuza maslahi ya watanzania na wazanzibar kupitia sekta ya habari na mawasiliano Tehema.
Pia dokta shein amesema manufaa makubwa yanayopatikana kutokana na matumizi ya sekta ya habari na mawasiliano ni kuchangia ukuaji wa uchumi katika nchi na kuwawezesha wananchi kuishi maisha bora na kuendana na mabadiliko ya dunia ya sayansi na technologia.
Akizungumzia uzinduzi mfumo wa usajili kwa kutumia mtandao wa kompyuta kwa tasisi za biashara na amana kwa mali zinazohamishika Dokta Shein Amesema mfumo huo mpya utawezesha wafanya biashara kutambulika kihalali na shughuli wanazozifanya.
Pia amesema kutarahisisha kupunguza gharama na muda kwa watoaji wa huduma na kuunganisha tasisi moja na tasisi nyingine kupitia mfumo huo mpya kwa kutumia mtandao.
Aidha amesema mfumo huo utawasaidia wafanya biashara wadogo wadogo kutambulikana kisheria na kuwarahisishia kupata mikopo ya kuwaongezea mitaji itakayo wasaidia kukuza biashara zao.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa wakala wa usajili biashara na mali zanzibar BPRA Abdallah Waziri Ramadhani amesema mfumo huo wa usajili kwa kutumia mtandao wa kompyuta kwa tasisi za biashara na amani kwa mali zinazohamishika kutasidia kutunza nyaraka na taarifa  zitokanazo na usajili.
Aidha amesema  lengo la kuanzisha mfumo huo wa usajili kwa biashara na mali  kustawisha biashara na mali kwa tija ya wazanzibar na watanzania kwa ujumla.
Nae waziri wa biashara na viwanda Zanzibar Amina Salum Ali amesema lengo la serikali ya Zanzibar kuhakikisha wanapunguza gharama na muda kwa wafanya biashara na kuwarahisishia kutambulikana kisheria.
Pia amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar watahakikisha wanaleta mazingira mazuri na mapinduzi ya  biashara kwa wafanya biashara nchini.
Mfumo huo mpya wa usajili kwa kutumia mtandao wa kompyuta kwa tasisi za biashara na mana kwa mali zinazohamishika umetengenezwa na kampuni ya NRD kutoka nchini Norway pamoja na kamati ya wataalamu wa IT kutoka katika tasisi za serikali ya mapinduzi ya zanzibar.
Uzinduzi huo ulifanyika katika ukumbi wa sheikh idrissa Abduli wakili kikwajuni mjini magharib unguja na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali, chama pamoja na dini.
Zanzibar24.

Comments