Rais msataafu wa awamu ya sita, Dk. Amani Abeid Karume, alieleza hayo wakati alipokua akizindua taasisi ya Love in Colors Foundation katika ukumbi wa Ngomekongwe mjini Unguja.
Dk. Karume alisema kwamba kila jambo lina muda wake, hivyo vijana hivi sasa ni wakati wao wa kuandaa mipango mizuri na kubuni mambo ambayo yataweza kuwaletea maendeleo yao na nchi kwa ujumla.
“Wakati tulipokua sisi vijana tulifanya mambo mbalimbali yanaonekana, hivi sasa tumeshakua watu wazima kwa hiyo huu ni wakati wenu na nyinyi vijana kufanya mambo ambayo mtakapokua watu wazima mje kujivunia kazi zenu,” alisema.
Dk. Karume alisema kwamba mtu yoyote akiwa na malengo anaweza kufika mbali na kuleta manufaa katika jamii, hivyo aliwataka vijana kujitahidi kubuni mawazo mazuri ambayo yatasaidia kujikwamua na tatizo la ajira na sio kusubiria ajira serikalini.
Zanzibarleo.
Comments