Benki
ya Dunia imeidhinisha mkopo nafuu wa Dola 350 milioni (zaidi ya Sh787.5
bilioni) kwa Serikali ili kuboresha miundombinu ya maji safi na salama.
Taarifa
ya benki hiyo iliyotolewa jana , Juni 27 inasema mkopo huo
utawanufaisha watu milioni tatu kupata maji safi na wengine milioni nne
wakiishi kwenye mazingira safi.
“Jana
bodi ya wakurugenzi wa Benki ya Dunia imeidhinisha mkopo huo
utakaoinufaisha mikoa 17 kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama
vijijini,” inasomeka taarifa hiyo.
Takwimu
zinaonyesha watu 11 katika kila 100 hupata maji safi maeneo ya vijijini
ambako ni shule moja kati ya kila mbili ina matundu ya vyoo yanayokidhi
mahitaji hivyo juhudi za ziada kuhitajika ili kuboresha miundombinu.
Kutokana
n ahali hiyo, watoto ndio wahanga wakubwa kwani takwimu zinaonyesha
mmoja katika kila watatu hukosa virutubisho muhimu yakiwamo maji ya
kutosha.
Kutokana
na mkopo huo, mkurugenzi mkazi wa benki hiyo, Bella Bird anasema kaya
1,250 na shule 1,500 zitanufaika kutokana na jitihada za Serikali
kuboresha huduma za umma.
“Ubora
wa rasilimaliwatu ni muhimu sana hasa kipindi hiki Tanzania
inapojipanga kuelekea uchumi wa kati. Upo uhusiano wa karibu kati ya
maji safi na salama na maendeleo ya afya ya mtoto hasa wa kike ambao
uhudhuriaji wao shuleni unalegalega nchini,” amesema Bella.
Mpekuzi.
Comments