
Akizungumza na waandishi wa habari huko
ofisini kwake Maisara Kaimu Mkuu kitengo cha uhusiano Khuzaimat Bakar
Kheir alisema ZURA ina kawaida ya kupanga bei kwa kuzingatia mambo
yafuatayo.
Alisema wastani wa mwenendo wa mabadiliko
ya bei za mafuta katika soko la Dunia (Platts Quatations ) katika mwezi
wa Machi , 2018 , kwa lengo la kupata kianzio cha kufanya mabadiliko ya
bei za mafuta kwa mwezi Mei ,2018.
Pia alisema gharama za uingizaji na
uhifadhi wa Mafuta katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na gharama za
kuyasafirisha tena hadi Zanzibar Vile vile gharama za Usafiri , Bima na ‘Premium ‘ hadi Zanzibar .
Thamani ya shilingi ya Tanzania kwa Dola , kodi ya Serikali na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejereja.
Kaimu huyo alisema Bei za mafuta kwa mwezi
Mei 2018 zimeshuka ikilinganishwa na bei za Mwezi wa April 2018 , sababu
za kushuka kwa bei ni .
Kushuka wastani wa mwendo wa mabadiliko ya bei za mafuta katika soko la Dunia (Platts Quatations ).
Kushuka kwa Gharama za uingizaji na
uhifadhi katika Bandari ya Dar es salaam pamoja na gharama za
kuyasafirisha tena hadi Zanzibar , hasa “Demurrage charges ambapo
mafuta ya Petrol yameshuka kwa Tsh . 5 kwa lita kutoka Tsh. 18.96 hadi
Tsh 13.98,mafuta ya Dizeli yameshuka kwa Tsh. 6 kutoka Tsh 21.08 kwa
lita hadi Tsh. 15.53 na mafuta ta Taa haijabadilika kwa mwezi wa Mei,
2018.
Kushuka kwa gharama za usafirishaji , Bima
na faida ya muagizaji (Premium) ambapo mafuta ya Petrol yameshuka kwa
Tsh . 49 sawa Asilimia 60% , mafuta ya Dizeli yameshuka kwa Tsh 8 sawa
na Asilimia 20% na Jet A-1(mafuta ya taa) haijabadilika.
Khuzaimat aliendelea kusema Bei ya reja
reja ya mafuta ya petrol kwa mwezi wa Mei, 2018 imeshuka kwa Tsh 89 kwa
lita kutoka Tsh 2, 344 ya Mwezi wa April ,2018 hadi Tsh hadi Tsh 2, 255
kwa lita katika mwezi wa Mei , 2018 sawa na punguzo la Asilimia 3%.
Bei ya reja reja ya mafuta ya Dizeli kwa
Mwezi wa Mei, 2018 imeshuka kwa Tsh. 64 kwa lita kutoka Tsh 2, 314 ya
Mwezi wa April , 2018 hadi Tsh 2, 250 sawa na Asilimia 2%.
Pia alisema bei ya reja reja mafuta ya taa kwa Mwezi wa Mei. 2018 haijabadilika ni Tsh 1.740 kwa lita.
Bei ya reja reja ya Mafuta ya Banka kwa
Mwezi wa Mei , 2018 imeshuka kwa Tsh 78 kwa lita kutoka Tsh . 2,156 kwa
lita katika Mwezi wa April, 2018 hadi Tsh, 2,078 katika mwezi wa Mei,
2018 sawa na punguzo la Asilimia 3%.
Na bei ya reja reja ya mafuta ya Ndege kwa
Mwezi wa Mei imeshuka kwa Tsh 2.5 kwa lita kutoka Tsh. 1,812.63 kwa lita
katika mwezi wa April , 2018 hadi Tsh 1,810.21 katika Mwezi wa Mei,
2018 sawa na asilimia 0.13%.
Bei ya reja reja ya Mafuta ya petrol itakua ni shilingi 2,255 kwa lita badala ya shilingi 2,344 ya hapo awali.
Bei ya reja reja ya Mafuta ya Dizeli itakua ni shilingi 2,250 kwa lita badala ya shilingi 2,314 ya hapo awali.
Bei ya reja reja ya Mafuta ya Taa itakua ni ile ile ya shilingi 1,740 kwa lita
Bei ya reja reja ya Mafuta ya Banka itakua ni shilingi 2,078 kwa lita badala ya shilingi 2,156 ya hapo awali.
Bei ya reja reja ya mafuta ya Ndege itakua ni 1,810.21 kwa lita badala ya shilingi 1812.63 ya hapo awali.
Zanzibar24,
Comments