Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
amezidi kumfagilia staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai kuwa
yupo Kwenye listi ya wasanii 10 duniani wenye Sauti nzuri.
Mwakyembe
amesema hayo kwenye mahojiano yake na kipindi cha KAA HAPA cha Mrisho
Mpoto na kueleza kuwa Diamond kwenye video zake hana haja ya kutumia
picha za ajabu ajabu kwani sauti yake ni dhahabu inajiuza.
“Kwenye tasnia yetu ya sanaa vijana wetu wanaimba nyimbo nzuri sana, wana vipaji vya hali ya juu.
"Kinacholeta
matatizo hapa ni picha ambazo haziendani na maadili yetu, kuchanganya
na utupu ndani yake hivi vitu kwa kweli wafanye wengine lakini sio
hapa.
"Tuchukulie
kijana kama Diamond sauti yeke pekee yake inatosha kabisa kumuuza.
Ukisema wasanii 10 duniani tuwe wakweli tuu! wenye sauti nzuri, Diamond
huwezi kumtoa pale.
"Lakini
huitaji kuuza ukaongeza na picha za ajabu ajabu wanaofanya hivyo ni
wale wenye mapungufu ili kuficha ma’flat flat kwenye nyimbo zao, Diamond
yeye haitaji kufanya hivyo”.
Suala
hili limekuja baada ya serikali kuingilia kati kazi za wasanii mbali
mbali na hata kufungia baadhi ya wasanii kama Roma Mkatoliki na baadae
kumfungulia.
Waziri
Mwakyembe amesisitiza kuwa serikali haina ugomvi wowote na wasanii bali
wapo katika jitihada za kulinda maadili ya nchi yetu.
Mpekuzi.
Comments