Kama alivyowahi kunukuliwa kwamba yeye
ni mpiga debe wa Tanzania ya Viwanda,jana Waziri Charles Mwijage
amehamishia debe hilo kwenye shule za sekondari akisema wanafunzi
waandaliwe kuchukua jukumu mbeleni kwa kuwa viwanda vinavyojengwa sasa
ni vile vya kipindi cha mpito.
Akihutubia
katika mahafali ya kidato cha sita kwa shule za sekondari Kaizirege na
Kemebos, jana Mei 19, Waziri Mwijage,alisema viwanda vya kudumu
vitajengwa na wanafunzi wanaoandaliwa vizuri katika masomo ya sayansi.
Alisema
kuwa wazazi na wanafunzi wanatakiwa kusoma upepo unapoelekea ambao
unawahitaji wanafunzi wa masomo ya sayansi kwa ajili ya kuchukua jukumu
la.kujenga uchumi wa viwanda.
Pia
aliwakumbusha wazazi na watu wenye mitaji wasikimbilie kwenye
uanzishaji wa viwanda vikubwa bali waanze na viwanda vidogo na baadaye
waende hatua kwa hatua hadi viwanda vikubwa.
Waziri
Charles Mwijage ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini
alikuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kudato cha sita shule ya
Sekondari Kaizirege na ya Kemebos ambapo jumla ya wanafunzi 180
wamehitimu.
Mpekuzi.
Comments