Na Othma Ali Juma –Pemba.
Jumla ya watoto 360 waliokatisha masomo na kujiingiza katika ajira za utotoni Shehia ya kiwani Mkoa wa kusini Pemba wamefanikiwa kurejeshwa Skuli na vyuoni baada ya wazazi wao kuamua kuanzisha ulinzi shirikishi(Polisi jamii).
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi huko kijijini kwao mmoja miongoni mwa polisi jamii Mohd Hamrani Awesi
amesema sababu iliyopelekea kuanzishwa kwa ulinzi shirikishi katika shehia yao
ni kutokana na madhila kuwa makubwa,kukithiri kwa ulevi,wizi pamoja na kundi
kubwa la watoto kukatisha masomo na kujiingizaa katika ajira mbaya za utotoni
za uvuvi.
''Ilifika wakati mpaka watoto ikawa
wanajenga kambi maporini kuiba kuku, kuvuta bangi na kufanya vitendo vengine
viovu ndipo tulipoona madhila yashakuwa makubwa tukaamua tuende kwa sheha
tukamshauri juu ya kuanzisha polisi jamii ikiwa lengo ni kupamba na watoto
wanaofanya matendo haya,pamoja na kuwarudisha skuli ili waendelee na masomo
yao,
“ tunamshukuru sheha alikisikia kilio
chetu na dipo alipokwenda kuzungumza na mkuu wa Wilaya kutoa taarifa na
akatuita wazee wote kutaka ridhaa zetu na tukaanzisha rasmi ulinzi
shirikishi''alisema Hamrani.
Amesema hadi kufikia sasa ambapo ni
takribani mieze 8 tokea kuanzishwa kwa ulinzi shirikishi wamefanikiwa kirejesha
skuli na vyuoni watoto 360 ambao tayari walikuwa washakatisha masomo.
Amesfahamisha kuwa licha kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa katika kuwatoa watoto katika ajira mbaya za utotoni lakini
hadi kufikia sasa bado kuna baadhi ya watoto hawajafanikiwa kuwarejesha skuli
hii ni kutokana na wazazi wao kutotoa ushirikiano wakutosha.
''Licha ya kazi kubwa tunayoifanya
ambayo inamaslahi kwa jamii na watoto wenyewe juu ya kapata haki yao ya msingi
ya Kielimu lakini wapo baadhi ya wazazi hawapendi kabisa kuona juhudi hizi
zinafanyika na wengine hadi kufikia kutupangia hujuma pamoja na vitisho
mbalimbali lakini sisi hatujali kwani lengo letu ni kuleta ukombozi kwa
jamii.'' ameeleza Hamrani.
Baadhi ya akina mama wa shehia hiyo
wamesema wanashukuru na sana kuanzishwa kwa polisi jamii kwani imekuwa
ikiwasaidia ulezi kwa kiasi kikubwa na kusema kuwa hadi sasa watoto ambao
tayari walikuwa wameshindikana wameweza kurejeshwa skuli na vyuoni.
''T unafurahikia sana kuanzishwa
polisi jamii mana watoto wetu wote walikuwa hawendi tena skuli wala chuoni,ukisema
nao hawasikiii, kabla ya kuanzishwa palisi jamii ilikuwa hapakai ndizi wala
kuku ukifumba macho ukifumbua kushaibiwa lakini sasa tunashukuru.''walisema
akinamama hao.
Kwa upande wake sheha wa shehia ya
Kiwani Abdallah Makame Hamad amesema moja ya malengo makuu ya kuanzishwa polisi
jamii ni kuhakikisha kila mtoto mwenye
haki ya kupata elimu anaipata na kusema kuwa katika shehia yake kuna tatizo
kubwa la kutokuwepo kwa vijana waliosoma.
''Tageti yetu kubwa ni suala la elimu
kwa sababu katika shehia yangu kumekuwa na upungufu mkubwa wa vijana waliosoma
unafika pahala unataka kijana aliyemaliza degree huwezi kumpata'' amesema sheha
huyo.
Ameeleza kuwa sasa wamepiga hatua
kubwa ya kimaendeleo kwani kundi kubwa la watoto waliotoroka skuli wamefanikiwa
kuwarejesha, kudhibiti masuala ya ulevi, watoto kwenda uchi pamoja na mikato ya
ajabu kwa vijana.
Amefahamisha kuwa licha hatua kubwa
ya maendeleo yaliyoipiga lakini pia kumekuwa na changamoto kubwa ambazo
zinaikumba polisi jamii na kusasababisha kutofikia malengo yake waliyojipangia
na kuzitaja kuwa ni pamoja na uhaba wa vifaa, kama vile tochi, usafiri, viatu
pamoja na kukosekana hata pesa kidogo kwa ajili ya watu wanafanya kazi hii ya
ulinzi shirikishi.
Aidha ameiomba serikali na taasisi
binafsi kujitokeza kuwaunga mkono kwa kuwasaidia kuwapatia vifaa vitakavyo saidia
kufikisha shebaha yao sambamba na hayo amewaomba wazee wale ambao hadi sasa
wanakuwa na fikra kuwa polisi jamii zinawaonea watoto wao kuachana na fikra
hizo potofu na badala yake kuungana kwa pamoja katika kuleta mabadiliko ya
kielimu katika sehia yao.
Comments