Spika
wa Bunge Job Ndugai amelazimika kuingilia kati mvutano ulioibuka
bungeni kuhusu tofauti ya bei ya sukari kati ya Tanzania Bara na
Zanzibar kwa maelezo kuwa majibu yaliyotolewa na Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage juu ya jambo hilo
hayajajitosheleza.
Kufuatia
sakata hilo, Ndugai amesema swali hilo litaulizwa tena wiki ijayo ili
Serikali itoe majibu ya kina, “hili ni swali la msingi sana na linapaswa
kutolewa majibu mazuri na Serikali.”
Mvutano
huo ulitokana na swali la mbunge wa Mpandae (CCM), Salim Hassan Turky
aliyehoji tofauti ya bei hizo na kujibiwa na Mwijage, majibu ambayo
mbunge huyo hakuridhika nayo.
Katika maelezo yake Mwijage amesema Tanzania Bara haina uhaba wa sukari na kuwatoa hofu watu mbalimbali.
Kuhusu
tofauti ya bei kwa pande mbili za muungano, waziri huyo amesema zaidi
ya asilimia 53 ya sukari itumikayo Zanzibar huagizwa kutoka nje kwenye
vyanzo ambavyo gharama zake ni nafuu ikilinganishwa na asilimia 29 ya
sukari inayoagizwa nje kwa upande wa bara.
Kufuatia
majibu hayo Ndugai amesema swali hilo halikujibiwa vyema. Katika swali
la msingi Jaku Hashim Ayoub (BLW) alihoji juu ya tofauti ya bei ya
bidhaa hiyo katika pande hizo mbili za muungano na kubainisha kuwa gunia
la kilo 50 visiwani Zanzibar linauzwa kwa Sh65,000 huku gunia hilo kwa
upande wa Tanzania Bara likiuzwa kwa Sh120,000.
Katika
majibu yake ya swali la msingi, Mwijage amesema wametoa maagizo kwa
viwanda vinne vya kuzalisha sukari nchini kuongeza ulimaji wa miwa
katika mashamba yake.
“Bei ya sukari ina maana kubwa kwa maisha ya Watanzania, haiingii akilini bei ya Tanzania Bara kuwa tofauti na ile ya Zanzibar.
"Kama
ni kweli wananchi wa Tanzania bara wanalipa sukari mara mbili ya ya
Zanznibar ili tu kulinda wenye viwanda....Haiwezekeni hiyo. Bunge
linahitaji majibu ya uhakika. " Amesema Spika Ndugai
Mpekuzi.
Comments