Serikali
kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema hakuna utaratibu
wowote unaoipa mamlaka Jeshi la Polisi kupiga raia au wageni kama baadhi
ya askari wanavyowafanyia wananchi bali kuna utaratibu wa kisheria
ambao unapaswa kufuatwa pindi raia au mgeni atakuwa amevunja sheria.
Kauli
hiyo imetolewa leo Mei 08, 2018 na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mhandisi Hamad Masauni Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 24
mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati
akijibu la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Ngara Alex Rafael Gashaza
ambapo alitaka kusikia kauli ya serikali juu ya kulipa fidia juu ya
wananchi wa Ngara na Tanzania kiujumla pindi wanapokamatwa na Polisi,
kupigwa na kisha kuja kubainika kuwa hawana hatia.
"Sio
utaratibu wa Jeshi la Polisi kupiga raia au hata wageni, kuna utaratibu
ikiwa mgeni au raia amevunja sheria anatakiwa uchukuliwe kwa mujibu wa
sheria, itabidi tukae tuchunguze kama kuna ukiukwaji wa sheria tuchukue
hatua za kisheria ili sheria ifuate mkondo wake", amesema Mhandisi
Masauni.
Kwa
upande mwingine, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi
Masauni amesema pindi hali ya kifedha itaruhusu wanampango wa kukarabati
kituo cha Polisi cha Ngara pamoja na nyumba za makazi za maaskari hao.
Mpekuzi.
Comments