Mwanamitindo Hamisa Mobetto amefunguka ni kwanini siku hizi hatokei tena kwenye video za muziki.
Hamisa
amesema kuwa ili aweze kutokea kwenye video ya wimbo wowote ule ni
lazima uwe mzuri zaidi ya Salome ya Diamond ambao video yake ndio ya
mwisho yeye kuonekana.
“Sifanyi
video tu nimefanya, ninachagua. Ninachagua wimbo, nachagua maudhui,
nachagua kila kitu, so for me kutokea kwenye video nyingine inabidi iwe
nzuri zaidi ya Salome,” amesema Hamisa.
Video
ya Salome kutokwa kwa Diamond Platnumz akishirikiana na Rayvanny
ilitoka September 18, 2016 na hadi sasa ina views Milioni 23 katika
mtandao wa YouTube.
Comments