Halmashauri
nchini zimetakiwa kuhakikisha zinaanzisha mifuko ya dawa na vifaa tiba
ili kurahisisha upatikanaji wa huduma katika Hospitali, Vituo vya Afya
na Zahanati katika maeneo yao.
Agizo
hilo limetolewa jana, Mei 2 na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika
hafla ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo, mkoani
Iringa.
Rais
Magufuli alisema kuwa kuanzishwa kwa mifuko hiyo kutasaidia upatikanaji
wa dawa na vifaa tiba kwa urahisi kwakuwa halmashauri zitakuwa na uwezo
wa kununua moja kwa moja kupitia fedha zitakazotokana na mifuko hiyo.
“Natumia
fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuanzisha mifuko ya dawa na
vifaa tiba (Drug Funds), hili isaidie katika kurahisha upatikanaji wa
dawa na vifaa tiba katika maeneo yenu”, alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.
Aliongeza
kuwa katika kutambua umuhimu wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba
Serikali imetenga Sh.50 Bilioni katika bajeti yake ya mwaka wa fedha
2018/19.
Mpekuzi.
Comments