Mwalimu
wa Sekondari ya Nyambureti wilayani Serengeti, anashikiliwa na polisi
kwa tuhuma za kumtorosha mwanafunzi wa kidato cha pili kwa zaidi ya siku
nne.
Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Juma Shija alikiri kushikiliwa kwa mwalimu huyo na kwamba alikamatwa Mei 2.
Hata
hivyo, mwalimu huyo amekana kuwa na uhusiano na mwanafunzi huyo na
kwamba hizo ni hila za baadhi ya watu kutaka kumharibia kazi.
Naye
mkuu wa wilaya hiyo, Nurdin Babu alisema mtuhumiwa anadaiwa kumtorosha
mwanafunzi huyo wakati wanatoka kwenye michezo ya Umiseta na kukaa naye
kwa siku nne.
“Mwalimu
hakuonekana kazini kwa siku nne na mwanafunzi halikadhalika, wazazi
wakaanza kumtafuta na baada ya kuonekana na kubanwa mtoto alieleza
alikuwa kwa mwalimu kwa kuwa ni mpenzi wake,” alisema Babu.
Babu
alisema baada ya mtoto kutoboa siri wazazi walikusanyika wakitaka
kumshambulia mwalimu huyo hali iliyoufanya uongozi wa wilaya kutuma
polisi ili kumnusuru na kumkamata ili aweze kueleza kwa undani.
“Mtoto
huyo anadai kuwa walianza uhusiano Oktoba 25, 2017 akiwa kidato cha
kwanza na kuwa mke wake akienda masomoni yeye anaendelea naye, kitendo
hiki hatuwezi kukivumilia lazima afikishwe mahakamani,” alisema.
Alisema wanaume wakware hawatavumiliwa kwa kuwa wanawaharibia watoto maisha yao.
Mkuu huyo wa wilaya alisema kwa mwaka jana zilikuwapo mimba zaidi ya 25 kwa shule za msingi na sekondari.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri hiyo, Juma Hamsini amemsimamisha kazi mwalimu
huyo kutokana na tuhuma hizo za utovu wa nidhamu na kuitaka polisi
kuhakikisha inamfikisha mahakmani.
Mpekuzi.
Comments