Ijumaa
Kenya inatarajiwa kuweka historia kwa kuwa na setilaiti ya kwanza
kuwahi kutengenezwa nchini humo itayotumwa katika sayari.
Chombo
hicho cha kuzunguka sayari kilitengenezwa na wanafunzi na watafiti wa
Chuo Kikuu cha Nairobi kwa ushirikiano na shirika la teknolojia za
sayari la Japan Space Agency (JAXA).
Naibu
makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Peter Mbithi amesema mafanikio hayo
ni dhihirisho ya hatua zilizopigwa nchini kuhusu utafiti wa kiteknolojia
ambao unaweza kuchangia katika maendeleo yatakayokuza uchumi wa
kitaifa.
Setilaiti
hiyo yenye ukubwa wa sentimita kumi kimchemraba itarushwa kwenye sayari
kutoka kituo kilichopo Japan, lakini Wakenya kadhaa watapewa nafasi
kushuhudia matukio hayo katika Chuo Kikuu cha Nairobi na yatarushwa moja
kwa moja.
“Kutakuwa
na tukio Japan, katika sayari na hapa chuoni kile kitakachofanyika
Japan kitashuhudiwa na baadhi ya Wakenya ambao watakuwa huko. Hapa
tutakuwa na hafla katika ukumbi ambako matukio yatarushwa moja kwa
moja. Tunasubiri siku hiyo kwa hamu,” amesema Profesa Mbithi.
Wale
ambao wangependa kuhudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa Chandaria
uliopo chuoni hapo, watahitajika kutuma maombi kwenye tovuti ya chuo
hicho na watafahamishwa kama wamebahatika kupata nafasi.
Profesa
Mbithi ameongeza kuwa setilaiti hiyo itatumiwa kukusanya data kuhusu
masuala mbalimbali muhimu kama mabadiliko ya hali ya anga, uhifadhi wa
wanyamapori, utabiri wa hali ya hewa miongoni mwa mengine.
Ametoa
wito kwa wadau wengine waungane nao ili kuimarisha zaidi utafiti kuhusu
masuala ya sayari, kutia nguvu chombo hicho ili kifanikiwe kutimiza
malengo yake.
Mkuu
wa taasisi ya mafunzo ya uhandisi katika chuo hicho, Profesa Jackson
Mbuthia amesema setilaiti hiyo yenye uzani wa kilo 14 itasafirishwa hadi
kwenye sayari mwendo wa saa saba mchana Ijumaa.
“Huu
ni mwanzo wa safari ambayo itawezesha Kenya kushiriki kwenye sayansi ya
sayari. Ni mara yetu ya kwanza kupiga hatua hii lakini tunaamini ni
muhimu katika ustawishaji wa sayansi nchini,” amesema.
Mpekuzi.
Comments