Kutokana na mabadiliko ya teknolojia kampuni ya Maxcom Africa imetangaza kuajiri wafanyakazi wapya wenye ujuzi unaohitajika.
Kutokana
mabadiliko hayo, baadhi ya wafanyakazi waliopo ambao ama nafasi zao
zitakufa kutokana na teknolojia mpya inayotumiwa na kampuni hiyo au
zitakuwa zinajirudia hivyo kuilazimu kuwapunguza.
Msemaji
wa Maxcom Africa, Deogratius Lazari amesema kwa sasa kampuni hiyo ina
watumishi 451 lakini baada ya Serikali kuanza kutumia mfumo wa
kielektroniki kwenye masuala mengi mfano utoaji wa zabuni, ukusanyaji wa
mapato na maeneo mengine, baadhi ya majukumu yamepungua huku mengine
yakizaliwa.
“Huwezi
kurundika wafanyakazi wengi kwenye eneo moja bila kujali tija yao.
Tulipunguza baadhi ya wafanyakazi walioonekana ufanisi wao upo chini
mwaka jana ila awamu hii ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia,”
amesema Lazari.
Amesema
yapo maeneo kadhaa ya operesheni za kampuni hiyo ambayo yameimarishwa
kiteknolojia kurahisisha majukumu ya menejimenti, wafanyakazi na
mawakala zaidi ya 15,000 waliopo nchini kote.
Taarifa
ya uwezekano wa kupunguza wafanyakazi wake iliyotolewa na mkurugenzi wa
uendeshaji wa kampuni hiyo, Charles Natai inasema utaratibu wa kisheria
utazingatiwa kufanikisha mchakato huo kwa wafanyakazi watakaolazimika
kupunguzwa. Taarifa ilitolewa Mei 4.
“Jambo
hili linatufanya sisi kufanya uamuzi wa kupitia upya mfumo wa
uendeshaji wetu na kuboresha miundombinu ya shirika ili kufikia mahitaji
yetu ya kibiashara wakati tukiimarisha ufanisi,” inasomeka sehemu ya
taarifa hiyo.
Mpekuzi.
Comments