Msanii
wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize ameingia Tena Kwenye vita ya maneno
na Ex girlfriend wake staa wa Bongo movie Jacqueline Wolper.
Tangu
jana kumekuwa na taarifa kwenye mitandao ya kijamii zilizomuonyesha
Wolper akimrushia Dongo Sarah ambaye ni mpenzi wa Harmonize kwa kumuita
Mlezi wa wana baada ya taarifa kusambaa kuwa kamtosa Harmonize na
kumchukua Mwarabu Fighter.
Baada
ya dongo hilo la Wolper, Harmonize alitokwa na povu zito kwani kwa
Kupitia ukurasa wake wa Instagram alimtetea mpenzi wake Sarah na kusema
yeye sio Mlezi wa wana ila Wolper ndo Mlezi wa Wana na kuambatanisha na
listi kamili ya wanaume wote aliokuwa nao Kwenye Mahusiano
Comments