Msanii
Harmonize amedai kuwa video ya faragha iliyovuja mtandao ikimuonyesha
Diamond akiwa na wanawake wawili ambao miongoni mwao alikuwepo Hamisa
Mobetto, ilikuwa ni sehemu ndogo ya movie waliyokuwa waki-shoot.
Harmonize
ameiambia Citizen Radio kuwa movie hiyo inalenga kuwafundisha wanaume
ambao wamekuwa na tabia za kuwadhalilisha wanawake.
“Walikuwa
wanashuti movie ambayo inaelezea wanaume ambao wanadhalilisha wanawake.
Sasa ili iweze kuleta attantion, ile iweze kulata item of bisness,
iweze kuleta value wakamtumia Diamond kama mtu ambaye ameshaonekana
katika mahusiano tofauti tofauti,” amesema Harmonize.
Utakumbuka
April 19, 2018 Diamond Platnumz aliomba radhi Watanzania kutokana na
kusambaza video hizo, hiyo ilikuwa ni baada ya kuitwa na Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) ambapo alisema kuwa amejifunza sheria za
makosa ya kimtandao na kuhaidi kutorudia tena.
Comments