
Maalim Seif alisema hayo katika mazungumzo na mkurugenzi wa taasisi
ya International Republican Insitute (IRI), Peter Alingo yaliyofanyika
makao makuu ya chama hicho Mtendeni mjini Unguja.
Alingo alikwenda kujitambulisha kama kiongozi mpya wa taasisi hiyo
baada ya mtangulizi wake kustaafu. makao makuu ya taasisi hiyo yapo
nchini Marekani.
Maalim Seif alisema CUF kikiwa chama cha siasa kitahakikisha
kinaendelea kuhubiri na kusimamia demokrasia kwa kuwa kinaamini uwapo
wake, ndiyo chachu ya mabadiliko ya utendaji ndani ya chama hicho na
Taifa.
Alisema wakiwa wadau wa haki na usawa watahakikisha wanamuunga mkono
kiongozi huyo mpya wa taasisi hiyo na wengine wenye malengo ya kusimamia
demokrasia na kuhubiri amani.
“CUF siku zote inaamini katika demokrasia ndiyo maana
tumekuwa na marafiki wengi kutoka asasi tofauti za kimataifa,
tutaendelea kuwa tayari kumkaribisha yeyote atakayetaka kushirikiana na
sisi,’’ alisema Maalim Seif.
Alieleza kusikitishwa na kile alichokiita kuminywa demokrasia nchini, ikiwamo vyama vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano.
Naye Alingo aliahidi kushirikiana na CUF na kwamba, bila uwapo wa
amani, hakuna kitu kitakachofanyika katika vyama vya siasa na Taifa.
Zanzibar24.
Comments