Msanii
wa Bongo Flava, Bonge la Nyau ametupa lawama kwa vyombo vya habari kwa
kile alichodai vinapendelea baadhi ya wasanii na kuacha wale wenye
vipaji vya kweli kama Q Chief.
Muimbaji
huyo amesema vyombo vya habari vimekuwa vikiangalia maslai binafsi
zaidi kuliko muziki wa msanii kitu ambacho kimekuwa kikiwaumiza wasanii
wengi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika mengi, hayo ni
baadhi;
"Kiukweli
kuna baadhi ya watu wameaminiwa na media kubwa na kupewa nafasi za
kupush muziki wetu ili uwafikie jamii ila wao ndio wamekuwa waharibifu
wakubwa wa huu muziki kwa kujenga matabaka na kuwagawa watu
"Leo
hii akitoa kazi huwezi kuiskia ikipewa nafasi kubwa kwenye radio wala
tv station kama baadhi ya wasanii wanavyopewa hiyo air time, ukiulizwa
utaambia Ohoo wakati wake umeisha, mara alikuwa mjeuri kipindi yupo juu.
"Wengine
watakwambia madawa yamemchanganya but ukiskiza kazi zake mpya ina ubora
kuliko hata hao wanaowaona wa maana kwa kipiki hicho.Wadau wamekuwa
wakiangalia sana biashara zao kulizo talent au kazi nzuri inayowafikia,
leo hii nyimbo haiwezi kutoka from no where na kufanya vizuri nchi nzima
kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya nyuma.
"Cha
kushangaza kingine chart ya mziki kwenye kituo A ni tofauti kabisa na
kituo B na C, hii inatugawa sana na inasababisha nyimbo nyingi zisiwe
kubwa atuwezi kufika kwa style hii, watu kuangalia maslai yao binafsi na
kujuana.
"Media
nyinyi ndo kila kitu kwenye huu muziki wetu bila ya nyinyi hakuna sisi,
hata mtu anapotokea kuteleza na kutofautiana nae yawapasa kumwangalia
tena kwa jicho la pili, Q chief anahitaji huruma yenu pia, ni kipaji na
msipoangalia ataangamia halafu tuanze kutafutana uchawi.
May
14, 2018 kulianza kuenea kwa taarifa kuwa Q Chief ameacha muziki na
alipotafutwa alieleza mengi ambayo anayapitia katika maisha yake kwa
sana pamoja na dhamira yake ya kutaka kuacha muziki.
Comments