Bajeti Wizara ya Kilimo mwaka 2018/19 yapigwa panga.

Waziri wa Kilimo, Charles Tizeba akizungumzaWaziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amewasilisha bajeti ya wizara yake mwaka 2018/19,  akiliomba Bunge liidhinishe Sh170.2 bilioni kwa mwaka 2018/19 ikiwa ni pungufu kwa Sh44 bilioni ikilinganishwa na bajeti ya wizara hiyo mwaka 2017/18.
Akiwasilisha bajeti hiyo bungeni leo Mei 15, 2018, Dk Tizeba amesema kati ya fedha hizo, Sh98.1 bilioni ni za kutekeleza miradi ya maendeleo, Sh64.1 bilioni ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Dk Tizeba amesema Sh28.6 bilioni ni kwa ajili ya mishahara ya wizara, Sh14.3 bilioni ni kwa ajili ya mishahara ya bodi na taasisi, Sh12.7 bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida kwa wizara na Sh8.5 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida kwa bodi na taasisi.
Katika bajeti ya mwaka 2017/18,  fungu 43 la Sekta ya Kilimo, iliidhinishiwa Sh214.8 bilioni. Kati ya fedha hizo Sh64.6 bilioni zilikuwa za matumizi ya kawaida na Sh150.3 bilioni kwa ajili ya maendeleo ambapo Sh59.6 bilioni fedha za ndani na Sh90.7 ni fedha za nje.
Mwananchi.

Comments