
Akikanusha madai hayo Afisa mdhamin Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Salum Kitwana Sururu amesema
kauli hiyo sio sahihi nakwambwa katika kipindi cha meizi mitatu iliyopita
Wizaraya hiyo imeweza kutoa ajira kwa walimu wapatao 248 ndani ya Wilaya zote
za Pemba kwa lengo la kuondokana uhaba wa walimu maskulini.
Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwakwe chake
chake Mh. Sururu amesema katika kuongeza
jitihada za kuleta walimu skuli ambazo bado zinaupungufu wa walimu wizara hiyo
itahakikisha tatizo hilo linafanyiwa kazi ili kuleta mafanikio yaliyo bora kwa
maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.
“Kuna baadhi ya viongozi wa kisisia wanadai eti wizara ya
elimu imeshindwa kuajiri walimu hasa kwa upande wa Pemba nahao waliowaajiri
hadi sasa ni walimu 8 nao wamepelekwa chokocho mimi nasema sikweli nakanusha
kauli hiyo maana kuanzia mwezi wa kwanza, wapili na watatu kwa mikataba tofauti
wizara yetu imeweza kutoa ajira za kutosha kwa wilaya zote za Pemba na
kusambazwa maneo tofauti tofauti ambazo zinaonekana kweli kuna upungufu”
Aidha amesema kuwa wanaendelea kuifanyia kazi kauli ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mh. Ali Moh’d Shein ya kuwataka kuondoa tatizo
lililojitokeza la upungufu wa walimu katika skuli mbali mbali hivyo bado jitihada hizo zinaendelea ili kuona kila skuli haileti
malalamiko yoyote ya walimu.
Hatahivyo amesema kuongezeka kwa kasikubwa ya uandikishwaji
wa wanafunzi na Walimu kustaafu
umepelekea kupungua Walimu kwabaadhi
maeneo hivyo kutoa nafasi kwa walimu wapya kuweza kuajiriwa.
“Tunaamini kuwa kuongezekwa kwakasikubwa ya uandikishwaji wa
wanafuzi ambapo kwa mwaka huu umeongezeka mara dufu, na walimu kufikia muda wao
wakustaafu kumeweza kuchangia hili pengo la upungufu wa walimu laki bado tumo
mbioni kuweza kuliziba lisije kuleta athar yoyote”
Comments