Msanii
wa Bongo movie Wema Sepetu amefunguka na kuweka wazi kuwa kamwe hawezi
kuigiza filamu moja na Mama mzazi wa Marehemu Steven Kanumba kwani
Mwenyewe hakutaka mama yake ajiingize Kwenye sanaa.
Wema
ameanika hayo huku akisisitiza kuwa kipindi wakati Kanumba yuko hai
alimweleza Wema ambaye alikuwa mpenzi wake kuwa kamwe hataki mama yake
ajiingize kwenye Bongo movie.
Wema
alifunguka hayo Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambao
walimuuliza endapo yupo tayari kucheza filamu na Mama Kanumba ambaye
hivi sasa amegeukia sanaa hiyo:
"Hapana,
siwezi kwa sababu Kanumba alikuwa hataki mama yake aigize na hata mimi
alishaniambia, sasa nitavunja makubaliano yetu mimi na Kanumba”.
Lakini
pia Kwenye mahojiano hayo Wema alikataa tuhuma alizorushiwa na Mama
Kanumba kuwa alipowenda nyumbani kwa Wema hakufunguliwa geti badala yake
aliishia kuchomeshwa mahindi:
"Jamani…kwanza siku hiyo mimi sikuwepo kabisa, niliambiwa tu alikuja na kwa nini nifanye hivyo sasa“.
Comments