
Hayo yamejiri baada ya wabunge hao kupinga mwongozo wa mwenyekiti kuwa mjadala kuhusu Muungano usiwepo kufuatia hoja ya Mbunge Frank Mwakajoka wa Chadema aliyedai kwamba Zanzibar haipati haki zake kwenye Muungano hasa kuhusu sakata la kuuza sukari Bara.
Kufuatia hatua hiyo, Mwenyekiti Mussa Azzan Zungu alilitaka bunge lisiendelee kujadili hoja hiyo ya Muungano mpaka atakapotoa majibu ya muongozo uliombwa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama.
Baadhi ya wabunge wa CCM nao walikuwa wameanza kutoka ndipo Mhagama akawasihi wabaki bungeni.
Aidha, Mbunge Saada Mkuya (CCM) amewataka wabunge kutoubeza Muungano kwani waasisi wake waliungana kwa spirit ya Umoja hivyo wasiibeze serikali badala yake waimarishe Muungano kwani una manufaa kwa pande zote.
chanzo:Zanzibar24.
Comments