Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imekanusha
taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa nauli
mpya zilizopangwa na mamlaka hiyo kwa safari za mabasi yaendayo mikoani.
Taarifa
hizo zilizosambazwa mitandaoni zimedai kuwa, uwepo wa nauli hizo mpya
za mabasi ya mikoani zimekuja kufuati kupanda kwa gharama za mafuta
(dizeli na petroli).
Taarifa
iliyotolewa na SUMATRA jana Aprili 14 kwenda kwa abiria, watoa huduma
na umma kwa ujumla, imeeleza kuwa, hakuna nauli mpya zilizotangazwa na
SUMATRA kwa sasa.
Aidha, wadau wanakumbushwa kuwa, viwango vya nauli kwenda maeneo mbalimbali ya nchi vinaweza kupatikana katika tovuti ya mamlaka hiyo ya www.sumatra.go.tz
Aidha, wadau wanakumbushwa kuwa, viwango vya nauli kwenda maeneo mbalimbali ya nchi vinaweza kupatikana katika tovuti ya mamlaka hiyo ya www.sumatra.go.tz
Aidha,
viwango hivyo vya nauli vinaweza kupatikana kupitia ujumbe mfupi wa
maandishi kwa kuandika neno Nauli (acha nafasi), sehemu unapoanzia
safari (acha nafasi), sehemu unapokwenda. Kwa mfano, Nauli Dar Tanga,
kisha tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.
chanzo:Mpekuzi.
Comments