Mtangazaji
wa Siz kitaa ya Clouds Tv anatarajia kufunga ndoa na video queen
maarufu Tunda ambae wamekuwa katika mapenzi kwa muda sasa.Casto anasema
kuwa kabla ya mwaka huu kuisha lazima atamuoa mwandada huyo.
"Unajua
nimekuwa na wanawake tofauti sana lakini kwa tunda nimekuta vitu
tofauti sana,kwangu naona anafaa kuwa mke wa mtu tofauti na watu wa nje
mnavyomuona. na nitamuoa kabla ya huu mwaka haujaisha."
Kuhusu
kuwa na mwanamke aliyepita katika mahusiano na wanaume wengi, Casto
anasema kwake yeye anaanzia pale alipoanza na Tunda na wala haangalii
kule nyuma alkopita kwa sababu hata yeye pia alishakuwa na wanawake
wengi.
"Alafu
kila unapokuwa na mahusiano na mwanamke na ukataka kujua wanaume
alikuwa nao yatakushinda.unachotakiwa kuangalia ni pale mnapoanzia tu.
Kwani hata mimi nilishakuwa nao wengi tu kabla ya lukutana na Tunda.
Comments