Trump amemtaja padri huyo aliyejulikana kwa jina la Andrew Brunson kama 'kiongozi wa kidini mwenye ustaarabu' na ambaye amefunguliwa kesi 'bila sababu zozote'.
Rais huyo wa Marekani amesema, "Eti wanasema yeye ni jasusi, lakini mimi ndio jasusi zaidi yake."
Aprili 16, kesi ya padri huyo ilianza kusikilizwa katika mji wa İzmir magharibi mwa Uturuki ambako kuna kanisa analoliongoza.
Brunson alitiwa mbaroni na maafisa usalama wa Uturuki mwezi Oktoba mwaka 2016 akiwa pamoja na mke wake.
Taarifa iliyotolewa na serikali ya Uturuki inasema kuwa, padri huyo alikuwa akiifanyia kazi harakati ya Fethullah Gülen, mtuhumiwa nambari moja wa jaribio la mapinduzi yaliyofeli ya mwezi Julai mwaka 2016 nchini humo.
Vilevile ametuhumiwa kuwa anashirikiana na chama cha Kikurdi cha PKK ambacho serikali ya Ankara inasema ni kundi la kigaidi.
Kesi ya Andrew Brunson anayetuhumiwa kufanya ujasusi dhidi ya serikali ya Uturuki itasikilizwa tena Mei 17.
chanzo:parstoday.
Comments