Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) iko katika hatua za mwisho kukamilisha upelelezi wa tuhuma
za ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Bilioni mbili zinazowakabili viongozi
wa kiwanda cha kukoboa Kahawa cha mkoani Kilimanjaro.
Viongozi
kadhaa wa kiwanda hicho kinachomilikiwa na Vyama vya Ushirika katika
Kanda ya Kaskazini wanatuhumiwa kuuza nyumba za ushirika kisha kununua
mtambo feki wa kukoboa Kahawa ambao haujafanya kazi tangu ununuliwe
miaka minne sasa.
Kaimu
Kamanda wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro, Moses Oguda amewaambia
waandishi wa habari kuwa baadhi ya majalada ya kesi hiyo yamerejeshwa
kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini kwa ajili ya utekelezaji.
TAKUKURU
pia imepokea taarifa za rushwa zipatazo kumi na tano na kuzifanyia
kazi, nyingi kati ya hizo zikiwa ni kutoka idara za Elimu, serikali za
mitaa, polisi na Mahakama.
chanzo:Mpekuzi.
Comments