Ametoa kauli hiyo wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliyehoji sababu za Bunge kushindwa kutoa gharama za matibabu za mbunge wa chama hicho Singida Mashariki, Tundu Lissu.
"Kuna siku nitataja orodha ya wabunge wanaotibiwa nje ya nchi. Ni lazima wawe na vibali hivi. Rais alishasema wazi kuwa anazuia safari za nje zisizokuwa na lazima.
Lissu alipelekwa Nairobi katika matibabu kwa utaratibu ambao haukuwa na kibali cha Bunge. Hili jambo nimeshalisema sana sijui kwanini linajirudia, "amesema na kuongeza:
“Nashukuru Lissu anaendelea na matibabu na ninajua kuna Wajerumani wanamsaidia."
Mwananchi.
Comments