Rais Rouhani aliyasema hayo jana Jumanne katika mazungumzo yake ya simu na mwenzake wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan na kubainisha kuwa, kuna umuhimu kwa Ankara na Tehran kuendelea kushirikiana na kushauriana ili kuimarisha usalama katika eneo la Mashariki ya Kati hususan Syria.
Rais wa Iran amesisitiza kuwa, "Katika hali ambayo, wakaguzi wa Shirika la Kuzuia Matumizi ya Silaha za Kemikali (OPCW) hawajatangaza matokeo ya madai ya kutumiwa silaha za kemikali mjini Douma, hakuna nchi inayoruhusiwa kufanya uvamizi wa kijeshi dhidi ya Syria. Kitendo hicho cha nchi za kibeberu cha kushambulia nchi zinayotaka na wakati zinapotaka, kimetia doa katika uhusiano wa kimataifa."
Kwa upande wake, Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema ili kulinda mipaka yote ya Syria na kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo kwa njia ya kisiasa, kuna haja nchi yake, Iran na Russia ziendelee kushirikiana ili kuimarisha jitihada za pande tatu.
Jumapili iliyopita, katika mazungumzo yake ya simu na Rais Vladimir Putin wa Russia, Rais Rouhani alisema kuwa, kitendo cha kibeberu cha Marekani cha kufanya mashambulizi dhidi ya Syria kimefichua jinsi Washington ilivyo na uhusiano wa moja kwa moja na magaidi.
Mazungumzo ya marais wa Russia na Iran yalijiri siku moja baada ya Marekani, Uingereza na Ufaransa kufanya mashambulizi ya kivamizi dhidi ya Syria.
chanzo:parstoday.
Comments