Dkt
Maria Kamm ndiye mwanamke wa kwanza wa Tanzania kupata Shahada ya
kwanza (Degree) na jana ametunukiwa tuzo ya heshima katika tuzo za
Malkia wa Nguvu zinazoandaliwa na Clouds Media.
Mama
Kamm ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Weruweru iliyopo
Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, akiwa kama Mzalendo wa kweli, ametumia
maisha yake kwa kiasi kikubwa kuwashauri na kuwaelimisha vijana katika
masuala mbalimbali ya Taifa.
Mgeni
Rasmi katika utoaji wa Tuzo hizo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Mwl Nyerere Posta jijini Dar, alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Ummy Ally Mwalimu.
chanzo:Mpekuzi.
Comments