Rais wa Zimbabwe amesema wameamua kushughulikia suala hilo ikiwa ni sehemu ya jitihada za serikali yake za kufufua uchumi wa nchi hiyo uliozorota katika miaka ya mwisho ya utawala wa Rais Robert Mugabe.
Akitoa hotuba kuu jana wakati wa maadhimisho ya uhuru wa Zimbabwe; maadhimisho ya kwanza kufanyika nchini humo bila ya Mugabe tangu nchi hiyo hiyo ipate uhuru mwaka 1980.
Rais Mnangangwa alikiri kuwa Zimbabwe ilifanya makosa na kuisababishia nchi hiyo kupoteza fursa za uwekezaji katika miaka ya karibuni.
Rais Mnangagwa aliye na umri wa miaka 75 alishika hatamu za urais mwezi Novemba mwaka jana kwa uungaji mkono wa jeshi ambalo lilionyesha upinzani wake kwa Robert Mugabe na kisha kumlazimisha kujiuzulu kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa Rais wa Zimbabwe anajaribu kurekebisha baadhi ya sera zilizokuwa zikitekelezwa na Robert Mugabe ambazo wawekezaji walizitaja kuwa zilikuwa zinakatisha tamaa kuwekeza huko Zimbabwe.
Zimbabwe inajiandaa kuendesha uchaguzi wa kwanza mwezi Julai baada ya kuondoka madarakani Rais Robert Mugabe; ambapo Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa atachuana na Nelson Chamisa kiongozi mpya wa chama kikuu cha upinzani nchini humo cha MDC.
chanzo:parstoday
Comments