
Hatua hiyo ni muendelezo wa kuongeza ufanisi wa bandari hiyo katika
kutoa huduma na kupunguza ushindani unaoupata kutoka katika bandari za
jirani za Durban na Mombasa.
Kwa siku za hivi karibuni serikali imekuwa ikifanya jitihada za
makusudi kupanua Bandari ya Dar es Salaam lakini pia kuongeza kina cha
maji ili iweze kuhudumia meli nyingi na kubwa zaidi. Hatua hiyo
itawezesha wateja wengi wa Tanzania na nje ya nchi kutumia bandari hiyo
kupitisha mizigo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari
Tanzania (TPA), meli hiyo ina uwezo wa kubeba makontena ya mizigo zaidi
ya 5,000 kwa wakati mmoja.
Akizungumza Bandarini DSM Mkurugenzi wa shughuli za Meli, Yusuph Mwingamnoamesema “Wasafrishaji
wa meli wanapenda kutumia meli kubwa kuepuka gharama, nikiwa na maana
kwamba Mombasa na Durban wao bandari zao ni kubwa wanaingiza meli kubwa
kuliko zinanzoingia DSM, maanake ni kwamba wafanyabiashara wengi
watakuwa wanachukua mizigo nje wanapeleka kwao, halafu sisi tuchukue
kwao kwa vimeli vidogo na vimeli vidogo vinalipa kidogo”
Hapa chini ni picha za meli hiyo;



Zanzibar24.
Comments